Advertisement

Responsive Advertisement

MIKOPO NA TOZO KWA WANANCHI


MAKATO YA BODI YA MIKOPO KWA ASILIMIA KUMI NA TANO(15%) NI MZIGO MZITO KWA MWANANCHI.

Bunge baada ya kuridhia ongezeko la MAKATO ya BODI YA MIKOPO kutoka 8% iliyopo kwenye mkataba hadi 15% ya sasa hakika imeleta changamoto kubwa ya hali ya kipato kwa wafanyakazi wanufaika hasa wale wa kipato cha kati na chini ambao ndiyo wengi Tanzania. Lakini pia changamoto imekuwa na makali zaidi kwa wafanyakazi wasio na posho nyinginezo bali mshahara pekee. Hapa nitaainisha mfano rahisi wa mfanyakazi asiye na posho kwa maana ya kuwa hulazimika kungojea mshahara pekee. Kidogo nimzungumzie mwalimu mwenye shahada moja.

Mwalimu wa Degree anayeanza kazi au aliyeanza kazi mwaka 2015 ana mshahara wa Basic Salary shilingi 716000/= ambapo asilimia 8% ya awali ni shilingi 57,280 na kwa sasa asilimia kumi na tano(15%) ni shilingi 107000/=

MAKATO KATIKA MSHAHARA KILA MWEZI 

1/Pension Fund (PSPF, LAPF, GEPF, NSSF nk) sh 35,800./=

2/Chama cha Walimu (CWT) Shilingi 14,320/=

3/Kodi ya Serikali (Income Tax)  shilingi 86,580/=

4/Bodi ya Mikopo shilingi 107000/=

5/Bima ya Afya (NHIF) shilingi 21,480/= 

JUMLA MAKATO KILA MWEZI NI SHILINGI 265180=

Katika MAKATO hayo inaonesha Bodi ya mikopo inakata MAKATO makubwa kuliko hata kodi ya Serikali (Income tax).. 

Hapo ukitoa shilingi 716000 - 265180=450820/= ndio Fedha anayobaki nayo Mwalimu wa Degree kwenda nayo nyumbani. 

Je Fedha hiyo ya sh 450820/= inatosha kwa matumizi ya Mwezi mzima kwa matumizi haya. 

1/Kodi ya Nyumba maana walimu hawana nyumba 

2/Maji, umeme na usafiri 

3/Mavazi kwa familia yaani watoto, mke /mme na yeye mwenyewe 

4/Chakula cha kutosha 

5/Mawasiliano kwa Mwezi 
Na matumizi mengine. 

Mwalimu huyo atajenga nyumba yake, kusaidia hata wazazi wake na kuwa na akiba kidogo ikizingatiwa Mwalimu hana posho yoyote wala semina yoyote tofauti na polisi, wanajeshi, manesi na madaktari miongoni mwa wengine?

Sijaijua dhamira na lengo la wabunge kuafiki mabadiliko haya ilihali wao ni wawakilishi wetu na wanazijua fika hali zetu za vijiji na miji tunayotoka? Je ni nani wa kumsemea common mwananchi ikiwa wawakilishi wetu wanakuwa sehemu ya kututia vitanzi shingoni. Au wabunge wanafikiri wanavyopokea mamilioni ya kodi zetu na posho na marupurupu lukuki na sisi walàlahoi tunapokea hayo? Ifike mahali wabunge watuwakilishe badala ya kulinda maslahi ya vyama vyao na nyadhifa zao.

I rest my case.(MR.PROGRAM)✍

Post a Comment

0 Comments