TENDA MEMA SIKU YA SABATO.
Mathayo 12:12
🦻Basi ni halali kutenda mema siku ya sabato.
Kulingana na amri ya nne Sabato iliwekwa wakfu kwa mapumziko na ibada ya kidini. Ajira zote za kidunia zilitakiwa kusimamishwa, lakini kazi za rehema na ukarimu zilikuwa kulingana na kusudi la Bwana. Hawakupaswa kuwekewa mipaka na wakati au mahali. Ili kuwasaidia walio taabika, kuwafariji walio na huzuni, ni kazi ya upendo inayoleta heshima kwa siku takatifu ya Mungu.
Mahitaji ya maisha lazima yashughulikiwe, wagonjwa lazima watunzwe, mahitaji ya wahitaji lazima yatolewe. Hatakosa kuwa na hatia yeye ambaye anapuuza kupunguza mateso ya watu siku ya Sabato. Siku takatifu ya pumziko la Mungu lilitengenezwa kwa ajili ya mwanadamu, na matendo ya huruma yanapatana kabisa na dhamira yake. Mungu hataki viumbe vyake viteseke kwa maumivu ya saa moja ambayo yangeweza kutolewa siku ya Sabato au siku nyingine yoyote ....
Sabato haijakusudiwa kuwa kipindi cha kutokuwa na shughuli isiyofaa. Sheria inakataza kazi ya kidunia katika siku ya kupumzika ya Bwana; riziki zinazofaidisha maisha lazima zikomeshwe; hakuna kazi kwa raha ya ulimwengu au faida halali siku hiyo; lakini jinsi Mungu alivyoacha kazi yake ya uumbaji, na kupumzika siku ya Sabato na kuibariki, vivyo hivyo mwanadamu anapaswa kuacha kazi za maisha yake ya kila siku na kutumia masaa hayo matakatifu kupumzika kwa afya, kuabudu, na matendo matakatifu. Kazi ya Kristo katika kuponya wagonjwa ilikuwa sawa kabisa na sheria. Iliheshimu Sabato.
Kazi ya kuwasaidia wanaoteseka ilitamkwa na Mwokozi wetu kuwa ni kazi ya huruma na hakuna kuhalifu Sabato.
Mahitaji ya wanadamu wanaoteseka kamwe hayapaswi kupuuzwa. Mwokozi, kwa mfano wake, ametuonyesha kuwa ni sawa kupunguza/kuondoa mateso siku ya Sabato.
UBARIKIWE UNAPOTAFAKARI 🙏🙏
0 Comments