✍🏻✍🏻 *KESHA LA ASUBUHI*
JUMAPILI: 15/08/2021
*SOMO: MBADALA WA KIUNGU*
_*Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. 2 Wakorintho 5:21.*_
*☑️Aliponya wengine; hawezi kujiponya mwenyewe" (15:31). Ni kwa sababu Kristo hakutaka kujiokoa mwenyewe ndio maana mwenye dhambi ana tumaini la msamaha au fadhila kwa Mungu. Ikiwa, katika kazi Yake ya kumwokoa mwenye dhambi, Kristo angeshindwa au kukatishwa tamaa, tumaini la mwisho la kila mwana na binti wa Adamu lingekuwa limefika mwisho. Maisha yote ya Kristo yalikuwa ni ya kujikana nafsi na kujitoa muhanga; na sababu ya kuwa na Wakristo imara wachache mno ni kutokana na kuendekeza na kujifurahisha nafsi kwao kuchukua nafasi ya kujinyima na kujitoa nafsi.*
_*☑️Lo, ni njaa na hamu iliyoje ya roho alikuwa nayo Kristo ya kuokoa kile kilochopotea! Mwili uliosulubiwa msalabani haukuondoa uungu Wake, nguvu Yake ya Mungu ya kuokoa kupitia dhabihu ya kibinadamu, wale wote ambao wangeikubali haki yake. Kwa kufa juu ya msalaba, alihamisha hatia kutoka katika nafsi ya mkosaji kwenda kwa Mbadala ule wa kiungu kupitia imani kwake kama Mkombozi wake binafsi. Dhambi za ulimwengu wenye hatia, ambazo kwa mfano zinaoneshwa kama "nyekundu kama damu," ziliwekwa kwa Mdhamini wa kiungu.*_☑️
_☑️Uungu ulikuwa ukifanya kazi yake wakati ubinadamu ulikuwa ukiteseka kutokana na chuki na kisasi cha watu wale wanaomchukia Mungu, kwa sababu Kristo likuwa amekiri kuwa Yeye ni mwana wa Mungu. Yeye peke yake alikuwa huru kuchukua udhamini wa mhalifu aliye na hatia ndogo kuliko wale waliomhukumu Yeye kufa, mwenye hatia kidogo zaidi kuliko makuhani, waandishi, na watawala ambao walishiriki kikamilifu katika kudai kifo cha Mwana wa Mungu._
_*☑️Ni imani iliyoje aliyokuwa nayo mwizi yule aliyekuwa katika kufa juu ya msalaba! Alimkubali Kristo wakati ilipoonekana haiwezekani kabisa Yeye kuwa Mwana wa Mungu, Mkombozi wa ulimwengu. Katika maombi ya mwizi yule masikini, kulikuwa na sauti tofauti
0 Comments