Advertisement

Responsive Advertisement

PROF. KITILA MKUMBO AUPONGEZA UONGOZI WA CLOUDS MEDIA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amepongeza uongozi wa Clouds Media Group kupitia Mkurugenzi wake Joseph Kusaga kwa kuendelea kutoa fursa kwa Watanzania hasa vijana ya kukuza biashara zao kwa kuzitangaza bidhaa zao kupitia vyombo vyake vya habari ambapo imesaidia kukuza biashara zao pia kutoa ajira.

Waziri Prof. Mkumbo ameyasema hayo Agosti 06, 2021 katika hafla ya kuwatambulisha Watanzania 55 ambao wameshinda nafasi 55 za kutangaziwa bure biashara zao kupitia Clouds Media Group kwa kila mmoja kutangaziwa matangazo yenye thamani ya shilingi milioni 10 ambayo kwa pamoja yatagharimu milioni 550 za Tanzania zilizotolewa na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga katika jitihada zake za kuwafungulia dunia Watanzania wenzake kupitia jukwaa lililofahamika kama “MCHONGO WA BIG JOE”

“Vijana wengi wana uwezo, kikubwa wanachokikosa ni fursa na nyie mmeweza kutoa fursa kwa watanzania 55 ambao mnaenda kuwakuza, hawa watakuja kuwa MaMillard Ayo wengine na watatengeneza makampuni mengine ambayo yatatoa ajira, maana ajenda kubwa ya Serikali ya awamu ya sita ni ajira kwa vijana” alisema Prof. Kitila Mkumbo

Aidha, Prof. Kitila Mkumbo ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara ili kuwapa nafasi ya kufanya ubunifu na uzalishaji ambao utasaidia kutengeneza makampuni mengi ambayo yatatoa nafasi kwa vijana kupata ajira na hatimaye biashara zao kukua.

Post a Comment

0 Comments