Advertisement

Responsive Advertisement

MAULID KITENGE APOKELEWA KWA MBWEMBWE EFM,

Hizi ni PICHA ya aliekuwa Mtangazaji wa Habari, Michezo na Mchambuzi wa Magazeti kutoka Wasafi Media, Maulid Baraka Kitenge sasa ni mwanafamilia wa EFM rasmi, akipokelewa na Mkurugenzi mkuu (CEO) Francis Ciza na Mchambuzi wa michezo Oscar Oscar.

"Nyumbani ni Nyumbani tu"---- KITENGE

Miaka ishirini (20) ya Baraka Kitenge kwenye tasnia ya Habari, tangu afanye kazi ITV, WASAFI MEDIA na sasa anarejea tena EFM.

"----->Tarehe 18 Octoba 2019, nilipost hapa Instagram kumuaga ndugu Maulid Kitenge ikiwa ni baada ya kukaa naye kwa takriban miaka 5, mimi na yeye tuliagana vizuri, tulitakiana heri, tuliachana kwa wema. Kwangu maisha yanapaswa kuwa hivyo"---- MAJIZZO

Aidha, amesema baada kukamilisha yaliyompeleka kule  Kocha Mchezaji Maulid Kitenge, anarudi tena hapa ambapo bila shaka ni nyumbani kwake. 

"----->Yeye ni kati ya watangazaji wa mwanzo hapa EFM, ni furaha kubwa sana kumkaribisha tena tufurahie pamoja hatua tulizofikia na kuendeleza mapambano zaidi."---- MAJIZZO

Post a Comment

0 Comments