*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumamosi, 07/08/2021.
*UTAMBUZI WA WAJIBU.*
*Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Ufunuo 3:17.*
▶️Je, ni nini kinachosababisha unyonge, uchi wa wale wanaojisikia kuwa ni matajiri na kuwa na mali nyingi? Ni ukosefu wa haki ya Krisito. Katika haki yao wenyewe wanawasilishwa kama waliovikwa nguo chafu, na bado katika hali hii wanajifurahisha wenyewe kwamba wamevikwa haki ya Kristo. Je, udanganyifu unaweza kuwa mkubwa zaidi ya huu? Kama inavyowakilishwa na nabii, wanaweza kuwa wakipaza sauti, "Hekalu la Bwana, hekalu la Bwana ndio haya" (angalia Yeremia 7:4), wakati mioyo yao imejaa biashara isiyo takatifu na mabadilishano yasiyo haki.
▶️Nyuso za hekalu la roho zinaweza kuwa maskani ya wivu, kiburi, shauku, dhana mbaya, uchungu, na urasimu usio na maana. Kristo huwaangalia kwa huzuni watu Wake wanaomkiri ambao wanajiona kuwa matajiri na kuongezeka katika maarifa ya ukweli, lakini bado ni mafukara wa ukweli katika maisha na tabia, na hawatambui hali yao ya ufukara. Katika dhambi na kutokuamini, wanadharau maonyo na mashauri ya watumishi Wake, na wanawatendea mabalozi Wake kwa dharau na aibu, huku maneno yao ya kukemea yanachukuliwa kama visa vya bure-visivyofaa. Utambuzi unaonekana kama vile umeondoka, na hawana uwezo wa kutofautisha kati ya nuru ambayo Mungu huwapelekea na giza linalokuja kutoka kwa adui wa roho zao.
▶️ *Yesu alipoondoka kwenda zake, alikabidhi kazi Yake katika nyanja mbalimbali kwa watu, na kila mfuasi wa kweli wa Kristo ana kazi ya kutenda kwa ajili yake, ambayo kwayo anawajibika kwa Bwana wake mwenyewe, na kazi hiyo anapaswa kuifanya kwa uaminifu, akisubiri amri na maelekezo kutoka kwa Kiongozi wake. Sisi ni mawakala wa Mungu wenye kuwajibika, na tumewekezewa mali za mbinguni, na tunapaswa kukaza macho kwa utukufu wa Yeye aliyetuita. Kwa upande wetu kunapaswa kuwepo na utekelezaji wa uaminifu wa wajibu, tukifanya kazi yetu iliyoagizwa kwa kiwango kamili cha uwezo tuliokabidhiwa. Hakuna kiumbe chochote hai kitaweza kufanya kwa ajili yetu ile kazi yetu. Tunapaswa kufanya kazi yetu kupitia katika matumizi ya bidii ya akili ambayo Mungu ametoa, tukiongezeka maarifa na ufanisi kadiri tunavyoendelea katika kazi yetu.*
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
0 Comments