• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / Covid19 / Habari / WATUMISHI 9 WASIMAMISHWA KAZI UWANJA WA NDEGE JNIA

    WATUMISHI 9 WASIMAMISHWA KAZI UWANJA WA NDEGE JNIA

    Bisaya Raphael July 13, 2021 Covid19, Habari
    Watumishi tisa wamesimamishwa kazi katika Kitengo cha upimaji wa COVID - 19 kwa wasafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA).

    Agizo hilo limetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi alipofanya ziara uwanjani hapo kukagua utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa juzi alipofika hapo akiwa ameambatana na Katibu mwenzake wa Wizara ya Uchukuzi.

    Prof. Makubi amesema hakufurahishwa na kitendo cha utovu wa nidhamu, kilichofanywa na watumishi cha kutokufika kazini bila kutoa taarifa rasmi kwa uongozi hapo jana na leo.

    "Jana watumishi wanane hawakufika na leo mmoja bila kutoa sababu ya msingi, jumla wanakuwa tisa," amebainisha.

    Ameongeza "Imeonekana hapa hili zoezi la baadhi ya watumishi kutokuja kazini limekuwepo, sasa hii imenisikitisha sana kwa baadhi ya viongozi kushindwa kuchukua hatua zinazostahili na kulindana kwa kuficha uozo.

    "Kwa hiyo hawa ambao hawakufika jana ambao jumla walikuwa wanane na kati yao wanne walikuwa wameajiriwa na Wizara ya Afya na wanne wameajiriwa na Manispaa ya Dar es Salaam, wapo chini ya RAS wa Dar es Salaam.

    "Nimeagiza hawa walio chini ya Wizara ya Afya wasimame kufanya kazi ili tufanye uchunguzi na kuchukua hatua stahiki.

    "Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu ambapo mtumishi anaamua kuacha kuja kazini na kusababisha usumbufu kwa wenzake na abiria ambao wanakuja hapa kwa sababu yeye 'gap yake haijawa covered' na mtu yeyote," amesisitiza.

    Prof. Makubi ameongeza "Lakini vile vile ambao wameajiriwa na Ofisi ya RAS nitashauri mamlaka husika nao wachukuliwe hatua hivyo hivyo ambazo zimechukuliwa kwa hawa wa Wizara.

    Amesema Serikali haiwezi kuvumilia watumishi wasio na nidhamu na wanaodharau majukumu wanayopewa.

    "Hizo ndizo hatua ambazo tumechukua, lakini pia tutahakikisha tutaleta wengine 'ku-replace' hao tisa waweze kuendelea ili tusije tukaathiri hizi shughuli za upimaji hapa 'airport'," amesema.

    Ametoa onyo kwa watumishi wa afya nchini, wawe tayari kufanya kazi popote pale watakapopangiwa.

    "Waende wakafanye kazi

    Related Posts

    Habari

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates