WATOA HUDUMA KUINGIA MIKATABA YA ULINZI WA MINARA
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew ametoa maelekezo kwa makampuni ya simu na wamiliki wa minara ya mawasiliano kuingia mikataba ya ulinzi wa minara ya mawasiliano na Serikali ya kijiji katika eneo husika
Mhandisi Kundo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Newala mkoani Mtwara ya kukagua ujenzi, uwezo na ubora wa minara ya mawasiliano ambapo alikutana na malalamiko ya malipo ya mlinzi katika mnara wa tigo uliopo katika Kijiji cha Mdimba pamoja na changamoto ya mawasiliano ya mtandao wa tigo kutokana na mnara huo kutumia nishati ya mwanga wa jua pekee
Sambamba na hilo, Mhandisi Kundo amewaagiza Wakuu wa Wilaya nchini ambao ndio wenyeviti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika maeneo yao kuhakikisha mtoa huduma yeyote mwenye mnara wa mawasiliano ndani ya wilaya zao anaandikiwa barua ya kufanya makubaliano mapya na kusainishana mikataba ya ulinzi wa minara na Serikali ya kijiji ambacho mnara upo
“Kuanzia sasa watoa huduma wote watakuwa wanaingia mikataba ya ulinzi wa minara na Serikali ya Kijiji husika ambayo ndio itawajibika kuhakikisha eneo la mnara linakuwa na ulinzi muda wote, utaratibu huu umekuwa ukitumiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) bila kuleta changamoto wala malalamiko ya aina yeyote”, alizungumza Mhandisi Kundo
Katika hatua nyingine Mhandisi Kundo ametoa miezi mitatu kwa kampuni ya simu ya tigo kuhakikisha imefikisha nishati ya umeme katika mnara wa mawasiliano wa kampuni hiyo uliopo katika kijiji cha Mdimba unaotumia nishati ya mwanga wa jua pekee wakati nishati ya umeme imekwishafika kijijini hapo
Aidha, katika ziara yake wilayani Newala Mhandisi Kundo amefanya ufuatiliaji wa minara ya mawasiliano ya kampuni ya simu ya Halotel iliyopaswa kujengwa kwa ruzuku kutoka Serikalini kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kukuta hakuna ujenzi wowote uliofanyika mpaka sasa ukizingatia kuwa mkataba wa ujenzi wa mnara wa Halotel katika kijiji cha Chilangala ulisainiwa toka Januari, 2020 na utekelezaji wake ulikuwa wa miezi 9 lakini hakuna utekelezaji wowote uliofanyika

Post a Comment