TENGENI MAPATO YA NDANI KUJENGA NYUMBA ZA WATUMISHI-SILINDE
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI David Silinde, amewagiza wakurugenzi wa halmashauri kote nchini kutenga fedha katika mapato yao ndani kwaajili kuboresha sehemu za kazi za watumishi kwa kujenga nyumba za watumishi, madarasa badala yakutumia fedha hizo kwa vitu ambavyo haviwagusi wananchi moja kwa moja.
Mhe. Silinde ameitoa kauli hiyo, baada ya kutembelea ujenzi wa nyumba sita za walimu ambazo zimejengwa na halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga katika shule ya msingi Tungulu ambayo walimu walikuwa wakiishi katika nyumba mbovu za udongo na kuchangia ufaulu mdogo wa wanafunzi wa shuleni hiyo.
Aidha Naibu waziri Silinde amesema ni aibu mpaka leo bado wanafunzi wanakaa chini au kwenye mawe darasani au kosomea chini ya miti kwa kukosa madarasa na kuagiza wakurugenzi ambao katika halmashauri zao kuna shida hizo watenge fedha kumaliza upungufu wa madawati na madarasa mapema iwezekanavyo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga na Mkurugenzi wa manispaa ya kahama Anderson Msumba, wameeleza sababu kubwa ya kufanikiwa kuwajengewa mazingira wezeshi watumishi wa manispaa ni kutengea fedha kila mwaka wa kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo nyumba na kuwawekea kila kitu ndani ili walimu wafundishe vizuri hata kama ni nje ya mji wajione kama wapo mjini na kwa mwaka huu wanakamilisha ujenzi wa nyumba zingine katika shule mbili za msingi.

Post a Comment