MAADILI NDIO IWE MSINGI WA KAZI ZENU-DKT. MAGEMBE

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Miko na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amewataka wafamasia kufuata maadili ya kazi zao ili kulinda heshima katika kada husika.

Dkt. Magembe ameeleza hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa bidhaa za Afya kwa wafamasia wa Mikoa na Halmashauri Julai 28, 2021 Jiji Dodoma.

Amesema wafamasia ni moja kati ya kada muhimu katika sekta ya afya ambayo inahitaji watendaji waadilifu na wenye uaminifu katika kutekeleza kazi zao.

"Wapo baadhi ya wanataaluma wachache wasio waadilifu na wanaharibu kwa kutokuwa waaminifu na kuharibu taaluma hiyo ambayo inategemewa katika mchango mkubwa kwenye Sekata ya Afya. Amesema Magembe, nakuongeza
‘’hata tukinunua dawa kiasi gani lakini kama hakuna usimamizi mzuri hatuwezi kupiga hatua’’ amesisitiza Naibu Katibu Mkuu huyo.

Katika hatua nyingine, ameweka wazi na kutoa maelekezo kupitia mafunzo hayo kwakuwataka wataalam wote wa Afya kuzingatia taratibu za serikali katika usimamizi wa bidhaa za afya na pale itakapobainika kuwepo na uzembe au ubadhilifu wa ukiukwaji wa taratibu, kisheria na kanuni ambazo zinaisababishia serikali kupata hasara hatua kali zitachukuliwa. Amesisitiza

‘’Ni jukumu la kila mmoja wetu aliyepo hapa kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma bora za dawa kulingana na miongozo ya tiba iliyopo’’ amesema Dkt. Grace

Vilevile amewawataka wakaguzi na maduka ya dawa kuwa na wajibu wa kutoa taarifa kwa Baraza na mamlaka wanazoshirikiana nazo wakiwemo Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA) kuhusiana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo inayohusiana na utoaji wa huduma na utendaji wa taaluma iwe kwenye sekta binafasi au ya umma

Naye Masajili wa Baraza la Famasia nchini Bi. Elizabeth Shekalaghe ameishukuru serikali kwakuongeza bajeti ya Afya na kuwahimiza wafamasia kusimamia maadili na kuipenda kazi yao kwa kujitoa kuitumikia vyema taaluma yao.

No comments