KENNETH MUGUNA ASAJILIWA AZAM FC

Klabu ya Azam FC Imemsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Kenneth Muguna, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia ya huko.

"Muguna anakuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu kwenye eneo la ushambuliaji, mkataba huo utamfanya kuitumikia Azam FC hadi mwaka 2023"---- AZAM FC

Kiungo huyo mshambuluaji ni miongoni mwa nyota wanaotamba kwenye soka la Kenya, msimu huu akifanikiwa kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Kombe la FA la nchini huko, iliyomalizika kwa timu yake ya Gor Mahia kuibuka mabingwa wa michuano hiyo.

Huu ni usajili wa nne kwa klabu ya Azam FC kuelekea msimu ujao, baada ya awali kuwasainisha nyota wawili kutoka Zambia, Charles Zulu, Rodgers Kola na beki wa kushoto Edward Manyama.

No comments