Mratibu wa Uhamasishaji Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa (BAVICHA), Bw. Twaha Mwaipaya amesema wameshinda hofu wamekataa woga.
Aidha, amesema hawakuruhusu kuona sheria inavunjwa.
"Tumelinda heshima ya Nchi yetu, hatukubali kutii amri batili ya Jeshi la Polisi kuahirisha Kongamano la Katiba Mpya Mwanza na tumetoka na msimamo wetu ni uleule hatuta ondoka Mwanza mpaka tufanye Kongamano."---- TWAHA MWAIPAYA
0 Comments