Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameweka picha na ujumbe ukitujuza kuhusu "Harmonize Europe Tour" ambayo inatarajiwa kuanza kufanyika tarehe 31 ya mwezi Oktoba mwaka huu 2021.
Ni mafanikio makubwa kwa msanii kuweza kupata matamasha haswa kwenye mataifa makubwa yaliyoendelea sana kwenye upande wa burudani.
Kwa Sasa msanii huyo anakimbiza kwa kibao chake kiitwacho Sandakalawe kilichotazamwa zaidi ya mara milioni 5.5 kwenye mtandao wa YouTube pekee ikiwa ni takribani wiki na siku chache tangu kiachiwe rasmi.
0 Comments