CHRISTIAN BENTEKE ATUA TANZANIA

Mshambuliaji wa kitamataifa wa Ubelgiji na timu inayoshiriki ligi kuu soka ya Uingereza ya Crystal Palace Christian Benteke yuko nchini Tanzania kwa Mapumziko ambapo leo tarehe 7/7/2021 ametembelea katika Hifadhi ya Ngorongoro kujionea utajiri wa Vivutio vilivyopo katika Hifadhi hiyo maarufu Duniani.

Ujio wa Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka nchini Ubeligiji ni kutokana na kuimarika kwa shughuli za utalii Nchini jambo ambalo linaendelea kusisitiza kuwa Tanzania ni salama kwa ajili ya shughuli za utalii kwa wageni.

No comments