Advertisement

Responsive Advertisement

AZAM FC WAMSAJIRI RODGERS KOLA AKITOKEA ZANACO ZAMBIA

Klabu ya Azam FC, imeingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa usajili huru akitokea Zanaco ya huko.

Mshambuliaji huyo mzoefu, mrefu na mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya kudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.

"Kola anakuja kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya ushambuliaji, kuanzia msimu ujao 2021/2022"--- AZAM FC

Aidha Kola ambaye wakala wake ni Nir Karin, akiwa Zanaco msimu uliopita, alifunga jumla ya mabao 14 katika mashindano mbalimbali nchini Zambia.

Post a Comment

0 Comments