Ndugu Sheha Mpemba Fakhi kwa tiketi ya CCM ameibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Konde wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.
"Ikumbukwe Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka kupitia taarifa kwa umma aliyoitoa hapo jana alieleza CCM inauhakika wa ushindi katika jimbo hilo na kata mbili zilizofanya uchaguzi hii leo kwa sababu ya aina ya wagombea iliyowasimamisha, aina ya kampeni walizofanya na mapokeo makubwa yenye hamasa yalioneshwa na wapigakura kwao"---- CCM
Aidha, CCM wamesema hili ni Jimbo la pili CCM kushinda tangu Sekretarieti mpya ya CCM ianze majukumu yake.
0 Comments