AMKA NA BWANA LEO 7

KESHA LA ASUBUHI

Jumatano 07/07/2021

*MATUNDA YA TOBA*

*Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi.* Mathayo 23:25

📚 Yohana alipokuwa akihuburi katika Jangwa la Yudea, na Mafarisayo na Masudakayo katika ubatizo wake, mhubiri huyo wa haki asiyeogopa aliwaambia hivi "Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira inayokuja? Basi zaeni matunda yapasayo toba" (Mathayo 3:7,8). Kwa kuja kwa Yohana, wanaume hawa hawakusukumwa na nia njema. Walikuwa wamepotoka katika kanuni na utendaji; laikini hawakujua hali yao halisi. Wakiwa wamejaa kiburi na tamaa ya makuu, hawangesita kuchukua njia yoyote  ambayo ingewawezesha kuwakweza nafsi na kuimarisha mvuto wao kwa watu. Na walidhani kuwa ubatizo kutoka kwa mwalimu huyu kijana maarufu ungeweza kuwasaidia katika kutekeleza hila hizi kwa mafanikio zaidi.

📚 Nia zao hazikufichika kwa Yohana, naye aliwakabili na swali kamilifu "Ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?" Laiti wangelisikia sauti ya Mungu ikiongea na mioyo yao, wangeliweza kutoa ushahidi wa ukweli huo wa kuzaa matunda yanayofaa toba. Hakuna tunda kama hilo lililoonekana. Walikuwa wamesikia onyo lile kama sauti tu ya mwanadamu. Walipendezwa na nguvu na uhodari ambao Yohana alizungumza nao; lakini hawakuwa wamesadikishwa na Roho wa Mungu, na kama matokeo ya hakika neno lililonenwa halikuzaa matunda kwa ajili ya uzima wa milele.

📚 Hakuna aliye mbali na ufalme wa mbinguni kuliko wale washika desturi wenye kujihesabia haki, ambao huenda wamejazwa na kiburi cha mafanikio yao binafsi, wakati ambapo wao ni fukara kabisa wa Roho wa Kristo, nao wanatawaliwa na husuda, wivu, na kupenda sifa na umaarufu. Wao ni wa tabaka ambalo  Yohana aliwaita kama uzao wa nyoka, watoto wa yule mwovu.Wanalitumikia kusudi la Shetani kwa ufanisi zaidi kuliko mpotovu aliyekithiri; kwa kuwa huyu wa mwisho hafichi tabia yake halisi; anaonekana kama alivyo hasa.

🔘 *Hakuna chochote pungufu ya maisha yaliyofanyiwa matengenezo-matunda yapasayo toba- yatakidhi masharti ya Mungu. Bila tunda kama hili, kukiri kwetu imani hakuna thamani.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

No comments