Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 18

*KESHA LA ASUBUHI.*

 *Jumapili, 18/07/2021.* 

*TALANTA ZILIZOKABIDHIWA KWA AJILI YA HUDUMA.*

" _Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;_ "
Warumi 12:5, 6.

▶️Mungu amempa kila mtu talanta kama amana. Kila mtu amempa kazi yake. Hakuwezi kuwa na watu wasio na kazi katika shamba lake la mizabibu. Kila mmoja ana kazi ya dhati kabisa, takatifu, makini ya kufanya kwa Bwana. Kwa kila mtu amekabidhiwa kazi ya kufanya, na hakuna anayeachiliwa. Siku ya hesabu ya mwisho itakuja, wakati Bwana atakapopiga hesabu pamoja na watumishi Wake. Mchungaji Mkuu ndiye Hakimu na anaonesha kanuni kuu ambazo zitapaswa kudhibiti utendaji wa kutoa hesabu pamoja na watumishi Wake ambao wamehesabiwa haki kwa imani, wakihukumiwa kwa matendo yao. Imani hufanya kazi kwa upendo na husafisha roho kutokana na unajisi wa kimaadili ili iweze kuwa hekalu la Bwana.

▶️Talanta zilizokabidhiwa hazijawekwa kwa ajili ya wachache vipenzi ambao wameinuliwa juu ya wenzao katika elimu, katika werevu wa akili. Vipaji ni zawadi zinazotolewa kwa familia ya Bwana kila mtu mmoja mmoja, kuanzia kwa watu wa hali ya chini kabisa na wasiojulikana kabisa hadi kwa wale walio katika nafasi za juu za dhamana. Karama zinazokabidhiwa zinawianishwa na uwezo wetu mbalimbali, na kila mtu anapaswa kutumia talanta hizi kwa utukufu wa Mungu. Anapaswa kuongeza kufaa kwazo kwa sababu kupitia katika kuzitumia anakuwa na sifa bora zaidi ya kufanya biashara. Nuru ya ukweli na faida zote za kiroho ni zawadi za Bwana. Zinapaswa kuthaminiwa na zinapaswa kuwa na mvuto katika akili na tabia. Tunapaswa kurudisha kwa Mungu ongezeko linalohusika, kulingana na karama tulizokabidhiwa.

▶️ *Tumechaguliwa kwa neema kama watumishi Wake. Mtumishi humaanisha mfanyakazi, yeye abebaye masumbufu, mizigo, wajibu.... Tunapaswa kutambua kuwa sio bidhaa zetu tunazofanyia biashara, bali ni mtaji tuliokabidhiwa na Bwana kwetu kuwekeza na kuukuza kama mawakili wenye busara wa bidhaa za Bwana wetu, ili tumrudishie mtaji wake pamoja na riba. Hatuwezi kuhodhi bidhaa za Bwana na tusifanye chochote; ndivyo alivyofanya mtumwa mvivu na shilingi yake na fursa zake alizopewa. Lazima aendeleze tabia, uwezo, kulingana na fadhila na fursa zake, ili kuwa mfanyakazi mkamilifu kwa ajili ya Mungu.*

Post a Comment

0 Comments