AMKA NA BWANA LEO 14
*KESHA LA ASUBUHI*
*JUMATANO, 14/07/2021*
*IMANI KAMILIFU*
" _Mtumaini Bwana kwa moyo wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe._ "
Mithali 3:5
▶️ Mungu ni msaada ulio karibu sana wakati wa mahitaji.Ikiwa utaweka tumaini lako kwake,atafanya wema wake upite mbele yako; Atakuongoza kwa mashauri yake. Roho wake Mtakatifu, majaliwa yake,mafundisho ya neno lake - Yote yatakuwa Wakala katika kufundisha na kukuongoza katika njia ya Bwana. Ahadi ya Mungu kwako ni," Sitakupungukia Kabisa,wala sitakuacha kabisa" ( Waebrania 13:5). Kwa hivyo unaweza kusema kwa unyenyekevu,Lakini kwa ujasiri thabiti, " Mungu huyu ni Mungu wangu milele na milele".
▶️Nimeagizwa kukuambia, "Usiitumainie nafsi, bali mtumaini Mungu. Hiki ndicho kipimo ambacho kwacho tunapimwa mbele ya mbingu - imani yetu kwa Mungu. Jitahidi kwa bidii kufanya kazi za Mungu.
Daima dumisha usahili wa utauwa wa kweli."Bali anikosaye hujidhuru nafai yake Mwenyewe " ( Mithali 8:36).Jifunze Maandiko; Kwani hakuna kitu ambacho kitaimarisha kabisa imani yako kwa Mungu au imani yako katika ukweli wake,kama hiki. Ikiwa utakuwa na imani kwa Mungu, huwezi kushindwa kuibuka mshindi.
▶️ Usizungumze juu ya majaribio na kukatishwa tamaa. Acha kuvitazama vitu hivi na Umwangalie Kristo. "Tazama Mwana- kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu" (Yohana 1:29). Wewe umenunuliwa kwa damu yake. Usimsikitishe Yule aliyetoa uhai wake ili upate kuwa mshindi. Alijaribiwa katika kila jambo ambalo wewe na mimi tunaweza kujaribiwa, na ili kustahimili alitumia usiku mzima katika maombi na ushirika na Baba Yake. Kristo hakuondoka hapa Ulimwenguni hadi alipofanya iwezekane kwa kila roho kuishi maisha ya imani na utii kamili, kuwa na tabia kamilifu.
▶️ Kristo alifanya iwezekane kwako wewe kuishi maisha yake. Unayo maneno Yake ya thamani kubwa katika Biblia;yaamini, tekeleza mafundisho yake. *Kamwe usitilie shaka neno la Mungu. Neno hili,kama litapokelewa maishani mwako,litakuadilisha na kukutakasa, na kuongeza kufaa kwako.*
▶️ *NI fursa yako kuwasaidia wale wanaohitaji msaada, kuzungumza maneno ya kutia moyo kwa wale wanaohitaji kutiwa moyo.Zingatia kuwa Unapaswa kuonesha kwa ulimwengu nuru ile ya utukufu wa Mungu.*
Post a Comment