AMKA NA BWANA LEO 12

*KESHA LA ASUBUHI.*

Jumatatu, 12/07/2021.

*PENDO LISILO KIFANI.*

*Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. Yohana 17:22, 23.*

*Ni upendo wa jinsi gani, upendo usio na kifani! Wanadamu walioanguka wanaweza kuunganishwa na Kristo kwa karibu kiasi kwamba wanatukuzwa pamoja Naye.* Katika dunia hii wamefuata nyayo zake, wakifanya kazi kwa bidii kama alivyofanya kwa ajili ya roho ambazo alizifia, na anapokuja kuwachukua walio wake, wataingia katika furaha Yake, wakikaa pamoja naye mezani Kwake katika ufalme Wake. "Nami nilipo" Anasema, "ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo". (Yohana 12:26).

Ni wazo zuri jinsi gani kwamba sisi, masikini, wenye dhambi tulioanguka, tunaweza kuwa kitu kimoja pamoja na Kristo, washiriki wa asili yake ya uungu, kupitia katika neema Yake iliyotakaswa, iliyosafishwa, iliyotukuzwa. *Tunaweza kushinda na kuketi pamoja na Kristo. Tunapaswa kufanana na sura yake. Yeye anatupenda, naye* atatusaidia. Tunapaswa kukaa tu mikononi mwake.

*Tunayo ahadi yake. Tunamiliki hati miliki ya mali isiyohamishika katika ufalme wa utukufu*. Kamwe hati miliki haikuandikwa kwa jinsi ya kushurutisha utii zaidi kulingana na sheria, au kutiwa sahihi iliyo dhahiri, kuliko zile zinazowapa watu wa Mungu haki ya makao ya mbinguni. *" Msifadhaike mioyoni mwenu," Kristo anasema: "mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo." (Sura ya 14:1-3)*

*Wale wote watakao wanaweza kuja kwa kupitia ahadi ya agano. Bei iliyolipwa kwa ajili ya ukombozi wetu ni ya thamani kubwa sana—damu ya Mwana wa pekee wa Mungu. Kristo alijaribiwa kwa uthibitisho dhahiri wa mateso. Asili yake ya kibidamu ilijaribiwa kabisa. Alibeba adhabu ya kifo kwa sababu ya dhambi ya mwanadamu. Akawa mbadala na mdhamini wa mwenye dhambi. Ana uwezo wa kuonesha mafanikio ya mateso na kifo chake, katika ufufuo wake kutoka kwa wafu. Kutoka kwenye kaburi lililopasuliwa la Yusufu linavuma tangazo, "Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Wale wanaoniamini mimi, na kutenda kazi za haki nizitendazo, wanahesabiwa haki, wanatakaswa, na kufanywa weupe na kujaribiwa. Wamepata utauwa na uzima wa milele."*

*MUNGU ATUBARIKI SOTE WAPENDWA.*

No comments