Takwimu zinaonesha takribani watu 10 kati ya 100 wana tatizo la ugonjwa wa Kisukari ambapo asilimia 60 ya wagonjwa wa ugonjwa huo hawajui kama wanaumwa.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.James Kihologwe wakati akizungumza kwenye mkutano wa Waganga Wakuu na Waratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza ambao walitoka katika Mikoa 26.
Dkt.Kihologwe amesema magonjwa ambayo yakuambukiza yamekuwa yakiongezeka nchini na takwimu zinaonesha kwamba watu 26 kati ya 100 wanamatatizo ya shinikizo la juu la damu.
Amesema takribani watu 10 kati ya 100 au asilimia 9 wanatatizo kubwa ka Kisukari ambapo amedai pamoja na ukubwa huu lakini takwimu zinatuonesha kwamba takribani asilimia 60 ya wagonjwa huo hawajijui kwamba wana tatizo la Kisukari.
Pia amesema watu 36 mpaka 22 wanamafuta mengi katika mishipa yao ya damu ambapo amedai zaidi ya robo tatu ya watu wenye shinikizo la juu la damu hajijui kama wana tatizo hilo.
“Lakini zaidi ya robo tatu ya watu wenye shinikizo la juu la damu hawajijui kama wanatatizo hilo unasikia tu mtu amenguka hajijui,”amesema.
Mkurugenzi huyo Msaidizi amesema matatizo hayo yamekuwa yakiongezeka kwa watanzania hivyo kupunguza maendeleo ya Nchi ambapo amedai katika kila asilimia 10 ya ongezeko la magonjwa hayo yamekuwa yakipunguza pato kwa asilimia 0.5.
“Tunasema katika kila asilimia 10 ya ongezeko la magonjwa haya linapunguza pato la Nchi kwani asilimia 0.5 na maana yake ni kwamba tutakuwa hatuna nguvu kazi ya kutosha katika maendeleo pamoja na gharama kubwa ya matibabu kwa wagonjwa,”amesema.
Amesema kutokana na ongezeko la magonjwa ambavyo sio ya kuambukiza,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imekuja na mpango wa kuhakikisha matitizo hayo yanapungua kwa kuja na mpango wa kubadili mtindo wa maisha ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.
Akifunga mkutano huo,Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,amesema Nchi imekuwa na mipango mikakati mingi ambapo amedai mingi imekuwa haiwasaidii watanzania.

0 Comments