SANAA NI BURUDANI-MWL. SUSAN NUSSU
Watazamaji na washiriki wote hatuna budi kusikiliza kwa makini ujumbe uliomo ili kuona ufundi uliotumika kuandaa nyimbo na ala zake za muziki pia kuona usanii ulio katika nyimbo zinazoimbwa na wanafunzi kutoka mikoa yote 26.
Kila mmoja baada ya mashindano haya atakuwa
amepata maarifa mapya yatakayomuwezesha
kujiandaa vema kwa ajili ya mashindano yajayo.
Tunatoa pongezi kwa walimu wote waliowaandaa wanafunzi hawa. Rai yetu ni kuendelea kuibua vipaji zaidi ili vijana wetu waweze kuwa na mafanikio zaidi ya kitaaluma na hata
kiuchumi maana fani za sanaa ya maonesho ni ajira.
----->Mkurugenzi msiadizi Ofisi ya Rais TAMISEMI, anayesimamia Elimu ya Awali na Msingi.
Post a Comment