RAIS SAMIA APOKEA MAPENDEKEZO KUIDHIBITI COVID-19
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 04 Juni, 2021 amepokea mapendekezo ya mpango kazi wa kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa kukabiliana na janga la ugonjwa wa Korona (Covid-19 na mapendekezo ya mpango kazi wa uratibu wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo yaliyowasilishwa na kamati ya wataalamu aliyoiunda kwa ajili ya
kuishauri Serikali juu ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Mapendekezo hayo yamewasilishwa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma nabMwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Said Aboud aliyeongozana na Wajumbe wa kamati Katika mapendekezo hayo, kamati imeshauri njia mbalimbali zitakazoiwezesha Serikali kupata fedha kutoka ndani ya bajeti ya Serikali na wadau mbalimbali wabmaendeleo yakiwemo mashirika ya Kimataifa na Sekta binafsi kwa ajili ya kughuramia
vifaa tiba, mafunzo na chanjo.
Mhe. Rais Samia ameipongeza kamati hiyo kwa kazi iliyoifanya na amemuelekeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima kuandaa andiko litakalowasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kujadiliwa na baadaye Serikali kufuya maamuzi kuhusu mapendekezo yaliyotolewa
na kamati.
Aidha, Mhe. Rais Samia amesema Balozi na Taasisi za kimataifa zimeruhusiwa kuleta chanjo za ugonjwa wa Korona kwa ajili ya kuwachanja raia na watumishi wake ili kuendana na taratibu za nchi zao na taasisi hizo pamoja na kuondoa kadhia wanazopata katika utendaji wa kazi zao kutokana na kutochanjwa.
Hata hivyo, Mhe. Rais Samia amesema chanjo hizo zitaletwa kwa utaratibu utakaoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Post a Comment