POLISI WAVURUGA MKUTANO WA UDA
Polisi Alhamisi walivuruga mkutano wa United Democratic Alliance (UDA) ulioitishwa katika hoteli moja Mombasa.
Kulingana na kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Nyali Daniel Masaba, walikuwa hawajafahamishwa juu ya mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Terrace Villas na kuhudhuriwa na miongoni mwa wengine Mwenyekiti wa UDA Johnson Muthama na Katibu Mkuu Veronica Maina.
"Hakuna mkusanyiko wa watu kama huu unaruhusiwa, haswa mkutano wa kisiasa," alisema kamanda wa polisi, akisisitiza kwamba mikutano ya kisiasa imesimamishwa kama sehemu ya hatua za kuzuia COVID-19.
Mkutano wa uhamasishaji ulikuwa umewakutanisha wagombeaji na wafuasi wa UDA kutoka mkoa wa Pwani.
Muthama, ambaye alikuwa akiongoza mkutano huo, alilazimika kutoroka baada ya maafisa wa polisi kuripotiwa kufika eneo hilo na kuwatawanisha wote.
Post a Comment