KENYA KUANZA KUTUMIA PASIPOTI KUSAFIRI

Wakenya sasa wataanza kutumia psipoti zao kusafiri, hii inafuatia kutiwa saini kwa hati ya makubaliano kati ya Posta Kenya na Idara ya Uhamiaji mnamo Alhamisi.

Pasipoti hizo zimetajwa kuwa zitahusika katika usafiri wowote mfano mabasi, ndege n.k

Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji Alexander Muteshi alisema mpango huo utapunguza safari nyingi zisizo za lazima na waombaji kwenda Nyayo House.

Kuanzia sasa, Wakenya watahitajika kufanya ziara moja katika ofisi za uhamiaji kuwasilisha nakala  ya maombi ili kufanikisha mpango wa kusafiri

Kwa upande wake, Mkuu wa Posta Dan Kagwe alisema ushirikiano huo utahakikisha huduma inayofaa kwa wakenya wote kupitia mtandao mpana wa Posta nchini na kupunguza mawasiliano kwa sababu ya janga la COVID-19.

Zaidi ya pasipoti 156,000 zimewasilishwa tangu kuanzishwa kwa huduma hizo mnamo Septemba 2020.

Mbali na pasipoti, huduma zingine ambazo zitatolewa kwa ushirikiano ni maombi ya kiotomatiki ya VISA, vibali vya kazi, uraia na kadi za wageni.

No comments