MTAKA, MAVUNDE WAUNGA MKONO JITIHADA ZA CHANG'OMBE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Anthony Mtaka sambamba na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mh. Anthony Mavunde wameunga mkono jitihada za wananchi wa Kata ya Chang’ombe za ujenzi wa kituo cha Polisi kwa kuchangia vifaa vya ujenzi na kuahidi kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa kuwashirikisha wadau wa maendeleo mbalimbali ili kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo hilo.
Hayo yamesemwa jana wakati wa Hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho cha Polisi lililowekwa na Mkuu wa Mkoa Mh. Anthony Mtaka na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katika kukamilisha ujenzi huo wa kituo cha Polisi,Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Waziri wake Mh George Simbachawene wamechangia Tsh 10,000,000,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kupitia kwa Mkuu wa Mkoa Mh. Anthony Mtaka Matofali 6700
yenye thamani ya Tsh 10,720,000 na Mbunge Mavunde aliyechangia saruji Tani 5 pamoja na rangi ya kupaka ya Thamani ya Tsh 1,000,000
“Nampongeza Diwani Fundikira na wananchi wote wa kata ya Chang’ombe kwa michango yenu ya ujenzi na kuona umuhimu wa kuwa na kituo hichi kwenye kata yenu.
Binafsi nimefarijika kuona utayari wa wananchi kwenye kutatua cha
gamoto zinazotukabili, pamoja na michango yetu tuliyoiahidi lakini mimi pamoja na Mbunge Mavunde tutahakikisha kituo hiki kinakamilika kwa wakati na kuwahudumia wananchi”Alisema Mtaka
Akitoa maelezo ya awali,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bw.Ramadhan Kailima amesema kituo hicho cha Daraja C kitakuwa ni kati ya vituo vikubwa katika Mkoa wa Dodoma ambacho kitakuwa na uwezo wa kuwa na askari 50 kama watoa huduma na hivyo kupongeza jitihada kubwa za wananchi na viongozi kujiletea maendeleo.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi,Mbunge Anthony Mavunde ameishukuru Wizara na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuwaunga mkono na kuahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa lengo la kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao katika Kata hiyo ya Chang’ombe.

Post a Comment