MAUA SAMA, CHEGE WATIA FORA UFUNGUZI WA UMISSETA
Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, wakiongozwa na Maua Sama pamoja na Chegge wamekonga nyoyo za wanamichezo wa UMISSETA na kuleta hamasa kubwa kwa wadau mbalimbali wa Sanaa mkoani Mtwara.
Wasanii hao wametumbuiza jukwaani leo Juni 2021 kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Caroline Nombo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Katika ufunguzi huo, vikundi mbalimbali vya kwaya na ngoma vimetumbuiza na kuufanya umati wa watazamaji kupanda jukwaani na kuimba pamoja na wasanii mbalimbali waliokuwawakitumbuiza.
Akisoma hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo Profesa Nombo amepongeza ubunifu wa waandaji wa mashindano ya mwaka huu kwa kuwashirikisha wasanii ili kuja kutoa burudani katika kipindi cha mashindano haya na kuonesha vipaji na vipawa walivyopewa na Mwenyezi Mungu.
“Pia ninawashukuru na kuwapongeza wasanii mbalimbali wanaoendelea kusherehesha wakiwemo Maua Sama na Chege, wasanii hawa wanasaidia kuitangaza michezo hii na wameongeza hamasa kwa jamii kuifuatilia nchi nzima wakiwemo wazazi, walezi wa wanafunzi na Viongozi wa Vyama vya Siasa na viongozi wa Serikali popote walipo”. ameongeza Profesa Nombo
Profesa Nomba alitumia ufunguzi wa mashindano hayo kuwaagiza wadhibiti ubora wa Shule kuanzia ngazi ya wilaya, kanda na Makao makuu ya Wizara kufanya tathmini na kutoa ushauri wa kuimarisha ufundishaji wa michezo, elimu kwa michezo na sanaa katika taasisi zote hapa nchini.
Katika kipindi hiki Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa shule zinatenga maeneo maalum kwa ajili ya michezo na Sanaa ili kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi.

Post a Comment