KILICHOJIRI KWENYE KIKAO CHA WAANDISHI WA HABARI
Kumekuwepo na taharuki baada ya mtu mmoja ambaye ameandika mambo ambayo hakuwa na uhakika nayo, alisema wanafunzi hawajachaguliwa kutokana na maombi yao bali na kazi iliyofanywa na TAMISEMI.
Kabla ya mitihani wanafunzi walijaza Selection Forms, kwenye Sel Form hizo walipaswa wajaze machaguzi matano kutokana na tahasusi ambayo kila mwanafunzi anatarajia kwenda kusoma.
Inapotokea pointi za chaguo lake la kwanza hazitoshi kuingia akiwa amepata ufaulu wa alama AAB, wengine wenye alama AAA wataingia chaguo la kwanza na mwenye AAB ataingia kwenye chaguo la pili.
Kuna wengine baada ya kukosa chaguzi kabisa tuliona sio vema watoto hao wakabaki nyumbani, hivyo tuliwapangia kwenye maeneo ambayo wanaweza kwenda kupata shule.
Kumekuwa na mawasiliano hafifu kati ya watoto na wazazi. Mtoto ameenda kumwambia mzazi kuwa chaguo lake la kwanza PCM wakati ukiangalia kwenye mfumo chaguo lake la kwanza ni PGM.
Niwaombe wazazi wenzangu tuwaeelekeze watoto wetu watuambie kile ambacho wao ndicho wamekichagua ili kuondoa dhana kwamba Serikali haijafanya kazi yake kikamilifu.
Wazazi ambao wanaona watoto wao hawajapata kile wachokiomba wawasiliane nasi kupitia call centre yetu, wapo wataalam mahususi watakaokueleza nini cha kufanya.
Tuna Maafisa Elimu kila Mikoa ná Wilaya na moja wapo ya kazi zao ni kupokea malalamiko, pelekeni malalamiko yenu hapo ili tuweze kutatua changamoto hizo. Niseme tu kwanza mfumo huu umekuwa wa uwazi ulioondoa rushwa, umepunguza na kuondoa matumizi ya fedha kwa wazazi katika kufatilia machaguzi ya watoto wao.

Post a Comment