Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda, 97, anapokea matibabu ya ugonjwa ambao haujafahamika katika hospitali ya jeshi katika mji mkuu Lusaka, ofisi yake ilisema Jumatatu.
Kaunda alitawala Zambia kutoka 1964, wakati taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza, hadi 1991.
Yeye ni miongoni mwa mashujaa wachache wa ukombozi wa bara hilo.
Msaidizi wake wa utawala Rodrick Ngolo alisema katika taarifa kwamba Kaunda amekuwa akihisi vibaya na amelazwa katika Kituo cha Matibabu cha Maina Soko huko Lusaka.
0 Comments