Mchezaji soka wa Kidenmark Christian Eriksen amewashukuru watu wenye mapenzi mema kutoka Duniani kote baada ya kuanguka uwanjani na kuufanya mchezo huo kusimamishwa kwa muda.
Kiungo huyo alichapisha picha yake akitazamia kutoka kitandani kwake hospitalini, akitoa kidole gumba.
Katika ujumbe uliochapishwa katika akaunti ya Twitter ya chama cha mpira wa miguu ya Denmark, amesema: "Asanteni sana kwa salamu zenu na ujumbe kutoka kote ulimwenguni. Ina maana kubwa kwa familia yangu.
"Kwa sasa Niko sawa kwa hali hiyo. Bado lazima nipitie mitihani hospitalini, lakini nahisi naendelea vizuri."
"Sasa, nitawashangilia wachezaji wenzangu wa Denmark kwenye mechi zijazo".
0 Comments