BALOTELI AWATAKA WAAFRIKA KUHAMA ULAYA
Nawahimiza wanamichezo wote wa Afrika tuchange pesa pamoja na mimi tuihame ulaya ya kibaguzi, tujenge viwanja vyetu na tuendeleze vipaji vya vijana wetu.
Tuna pesa tunaweza kujenga angalau viwanja vitano vyenye ubora kwa kila nchi na kufanya mchezaji wa kiafrika asitamani kamwe kwenda ulaya.
Hapa Afrika watacheza kwa umoja mbele ya ndugu zao bila kusikia maneno yoyote ya kibaguzi Afrika tuna vipaji.
Tunaweza kufanya ligi yetu ya mabingwa (champions league) iwe bora na ligi zetu pia ziwe bora....afrika tuna vipaji lakini kamwe havijawahi kukubalika nje ya bara letu"
Post a Comment