SYLVAIN ORE KUMALIZA MUDA WAKE MEI 31

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan Jana tarehe 27 Mei, 2021 amekutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Sylvain Ore ambaye anamaliza muda wake tarehe 31 Mei, 2021.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Rais Samia ameipongeza Mahakama hiyo ambayo
makao yake makuu yapo Jijini Arusha, Tanzania kwa kazi inazozifanya na amemhakikishia Mhe. Ore kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kushughulikia changamoto mbalimbali kwa kuwa inatambua umuhimu wa majukumu yake.

Aidha, Mhe. Rais Samia amempongeza Mhe. Ore kwa utumishi wake wa vipindi viwili vya Urais wa Mahakama hiyo na amemuomba kuendelea kuwa balozi mwema wa Tanzania.

Kuhusu Tanzania kufuta tamko la kuruhusu taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) na watu
binafsi kupeleka mashauri yao moja kwa moja katika Mahakama hiyo, Mhe. Rais Samia
amesema Tanzania italiangalia jambo hilo lakini kwa sasa msimamo haujabadilika.

Kwa upande wake, Mhe. Ore amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa ushirikiano ambaobMahakama hiyo imeupata kwa kipindi chote cha uongozi wake, na amemhakikishia kuwa Tanzania sehemu sahihi ya Mahakama hiyo kuwepo kutokana m uwepo wa amani, utulivu na mandhari ya kuvutia.

Mhe. Ore ambaye ametumia fursa hiyo kumunga Mhe. Rais Samia amebainisha kuwa katika kipindi cha uongozi wake Mahakama imeendelea kutekeleza majukumu yake vizuri katika kufikia matarajio ya Bara la Afrika na kwamba amefurahi kupata nafasi ya kumueleza Mhe. Rais Samia kuhusu Mahakama hiyo.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

No comments