Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 22 Mei, 2021 ameningumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masauja Kadogosa kuhusu maendeleo ya miradi ya ujenzi wa reli na maendeleo ya TRC.
Katika mazungumzo hayo, Bw. Kadogosa amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa Serikali
ya Awamu ya Sita kuidhinisha kiasi cha shilingi Bilioni 372.31 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kipande cha 5 cha reli ya Mwanza - Isaka chenye urefu wa kilometa 311 kwa kiwango cha kisasa (standard gauge rail).
Bw. Kadogosa ameelea kuwa tangu Mhe. Rais Samia aingie madarakani ujenzi wa reli katika vipande 2 unaendelea vizuri ambapo hadi mwezi uliopita kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (hikmet 3000 kilikuwa kimefikia ya asilimia 91 na Morogoro - Makutupora kilometa 129 kilikuwa kimefikia asilimia 60.02.
Amebainisha kuwa majaribo ya treni ya abirin yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi
Agosti, 2021 kwa kipande cha Dar es Salaam - Morogoro Kwa upande wake, Mhe. Rais Samia amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria
kuhakikisha ujenzi wa reli ya kati utakaounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi unakamilishwa ili kuzifikia nchi za Uganda,
Burundi, Rwanda na DRC, Amemtaka Bw. Kadogosa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ya ujenzi vizuri ikiwa ni pamoja na kujipanga kwa ajili ya ujenzi wa vipande vya Makutopora - Tabora, Tabora Isaka na Kaliua - Mpanda - Kalema.
Mhe. Rais Samia ameipongeza TRC chini ya Bw. Kadogosa pamoja na wote wanaoshiriki
katika tijenzi wa reli kwa kazi nzuri wanayoifanya na ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya miradi hiyo.
0 Comments