Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb) ameongeza siku 5 kwa waombaji wa kazi za Elimu na Afya hivyo kwa sasa mwisho wa kuomba ajira hizo ni tarehe 28 Mei, 2021 na sio tarehe 23 Mei, 2021 kama ilivyotangazwa hapo awali.
Mhe. Ummy ameongeza siku hizo ili wale wote walioshindwa kukamilisha maombi yao tangu Ajira hizo zilipotangazwa tarehe 09 Mei, 2021 kwa sababu zozote zile kutumia muda huu wa nyongeza kukamilisha maombi hayo kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz
Aliongeza kuwa mpaka tarehe 21.05.2021 saa 5:59 usiku waombaji wapya waliojisajili kwenye mfumo kwa kada ya Afya ni 49,951 na Elimu 20,975 huku waliohakiki taarifa za awali kwa kada ya Elimu ni 78,808 na kwa jumla sasa maombi yote yaliyopokelewa kwa ukamilifu kwa kada ya Afya ni 31,673 na Elimu ni 89,958.
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ilipata kibali cha ajira za Watumishi
wa kada mbalimbali za Afya 2,726 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na Walimu 6,949 wa shule za Msingi na Sekondari watakaofanyabkazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Waombaji walitakiwa kutuma maombi kuanzia tarehe 09-23 Mei, 2021 hivyo kwa sasa
mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 28 Mei, 2021.
0 Comments