wa Wakuu wa Mikoa watendaji wakuu wa taasisi kama ifuatavyo:
anachukua
1. Amemteua Bw. Anthony John Mtaka kuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mtaka alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
2. Amemteua Bi. Zainab Rajab Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Kabla ya uteuzi huo Bi. Telack alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na anachukua nafasibya Bw. Godfrey Zambi ambaye amestaafu.
3. Amemteua Mhandisi Robert Gabriel Lubumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Kabla ya uteuzi huo Bw. Luhumbi alikuwa Mkuu wa Geita.
4. Amemteua Bw. Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mbeya. Kabla ya uteuzi huo Bw. Homera alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
5. Amemteua Bw. Martin Reuben Shigella kuwa Mku wa Mkoa wa Morogoro Kabla ya uteuzi huo Bw. Shigella alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga
nafasi ya Bw. Loata Erasto Ole Sanare ambaye amemaliza muda wake.
6. Amemteua Mej. Jen. Marco Elisha Gaguti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi huo Mej. Jen. Gaguti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na anachukua nafasi ya Bw. Gelasius Gasper Byakuwa ambaye atapangiwa majukumu mengine.
7. Amemteua Bw. Albert Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Kabla ya uteuzi huo Bw. Chalamila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
8. Amemteua Bw. Aboubakar Mussa kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Kabla ya uteuzi huo Bw. Kunenge alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Mhandisi Evarist Welle Ndikilo ambaye amestaafu.
9. Amemteua Bw. Joseph Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mkirikiti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na anachukua nafasi ya Bw. Joachim Leonard Wangabo ambaye amestaafu.
10. Amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mahenge alikuwa Mkini wa Mkoa Dodoma na anachukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amestaafu.
11. Amemteua Dkt. Philemon Rugumiliza Sengati kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Sengati alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
12. Amemteua Bw. John Vianney Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mongella alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
13. Amemteua Bw. Ally Salim Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Kabla ya uteuzi huo Bw. Hapi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
14. Amemteua Bw. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Kabla ya uteuzi huo Bw. Malima alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
15. Amemteua Bw. David Zacharia Kafulila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Buv. Kafulila anachukue nafasi ya Bw. Idd Hassan Kimanta ambaye amestaafu.
16. Amemteua Bw. Amos Gabriel Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Bw. Makalla machukua nafasi ya Bw. Aboubakar Mussa kumenge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani. .
17. Amemteua Bi. Rosemary Staki Senyamule kina Mkuu wa Mkoa wa Geita. Bi. Senyamule anachukua nafasi ya Bw. Robert Gabriel Lathumbi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
18. Amemteua Bi. Queen Cuthbert Sendiga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Bi. Sendiga anachtikua nafasi ya Bw. Ali Salim Hapi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Tabora.
19. Amemteua Brig. Jen. Charles Mbuge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Bw. Mbuge anachukua nafasi ya Mej. Jen. Marco Elisha Gaguti ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
20. Amemteua Bi. Mwamu Mrindoko kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi. Bi. Mrindoko anachukua nafasi ya Bw. Juma Zubeir Homera ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
21. Amemteua Bw. Stephen Kagnigai kuwa Mkını wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huo Bw. Kagaigai alikuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anachukua nafasi Bi. Anna Elisha Mghwira ambaye amestaafu.
22. Amemteua Brigjen. Wilbert Augustine Ibuge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Brig. Jen. Ibuge anachukua nafasi ya Bi. Christine Mndeme ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM.
23. Amemteua Bw. Omay Tebweta Mgumba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Bw. Mgumba anachukua nafasi ya Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ambaye amestaafu.
21. Amemteua Bw. Makongoro Nyerere kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Bw. Makongoro Nyerere anachukua nafasi ya Bw. Mkinikiti ambaye ameteuliwa kuwa Mkini wa Mkoa wa Rukwa.
25. Amemteua Bw. Thobias Emir Andengenye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
26. Amemteua Bw. Marwa Mwita Rubirya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Bw. Rubirya anaendelea na wadhifa huo huo katika Mkoa huo htio wa Njombe.
Mhe. Rais Samia amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa taasisi zifuatazo;
1. Amemteua Mhe. Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mhe. Balozi Sokoine anachukua nafasi ya Brig. Jen. Ibuge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Ruvuma
2. Amemteua Bi. Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bi. Mwihambi anachukua nafasi ya Bwv. Stephen
Kagaigai ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
3. Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuna Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bw. John Nguya ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
4. Amemteua Bw. Sylvester Antony Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Mwakitalu anachukua nafasi iliyoachwa na Bw. Biswalo Mganga ambaye ameteuliwa kuwa Jaji
wa Mahakama Kuu.
5. Amemteua Ber. Joseph Pande kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (DDPA. Bw. Pande anachukua nafasi ya Bw. Edson Athanas Makallo ambaye atapangiwa majukumu mengine.
6. Amemteua Kamishna Msaidizi wa polisi (ACH) Salum Rashid Hamduni kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU). ACP Hamduni anachukua nafasi ya Brig. Jen. John Mbungo ambae atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Mhe. Rais Samia amempandisha cheo ACP Hamduni kuwa Kamishna wa Polisi (CP).
7. Amemteua Bi. Neema Mpembe Mwakalyelye kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU.
0 Comments