Huyu ndiye Lengai Ole Sabaya Jambazi aliyejificha kwenye kivuli cha ukuu wa wilaya na kulindwa na mamlaka za nchi. Mtu aliyewahi kughushi kitambulisho cha idara ya usalama wa taifa, na kushtakiwa mahakamani lakini bado akapewa ukuu wa wilaya. Unampaje uongozi mtu mwenye 'jinai' ya kughushi?
Ajabu ni kwamba kila alipoulizwa kuhusu tuhuma zake alikimbilia kumtaja Mbowe. Nikajiuliza je Mbowe ndiye alimtuma kuteka watu? Mbowe ndiye alimtuma kumvamia Nandy hotelini? Mbowe ndiye alimtuma aweke namba za UN kwenye magari yake ya kufanyia ujambazi? Mbowe ndiye alimtuma ampige diwani wa Sombetini? Kwanini kila anapoulizwa anamtaja Mbowe?
Nikagundua hii ndio njia aliyokua akiitumia kumhadaa mwendazake. Alikua akifanya ukatili anajificha kwenye kivuli cha Mbowe na upinzani. Na mwendazake alimuelewa maana upinzani ulikua adui yake mkubwa. Ukiteka, ukijeruhi, ukiharibu mali ya mtu we sema unafanya hivyo ili kuumaliza upinzani, mwendazake atakuelewa.
Kwahiyo Sabaya alisahau kwamba zama zimebadilika. Ndio maana juzi alipokua CMG alimtaja Mbowe mara nyingi zaidi kuliko tuhuma zinazomkabili. Alidhani kwa kusema amemng'oa Mbowe itamsaidia kujustify maovu yake, kumbe mama ana hofu ya Mungu na hapendezwi na huo uzandiki.
Suala hili la Sabaya lisaidie media kuzingatia profesionalism. Ni aibu media kubwa kama CMG kutumika kumsafisha "jambazi" Sabaya. Ile interview ya juzi ilikua "biased" na ilikosa impartiality and objectivity. Hata Sabaya alivyokua ana-behave sio kama interviewee, bali kama bepari aliyenunua kipindi, akajiandalia maswali na hivyo anajibu anavyojisikia.
Kaka mkubwa @edokumwembe aliwahi kusema "Heshimu watu, sponsor hufariki" nadhani hili ndio somo ambalo kila kiongozi anapaswa kujifunza kwa Sabaya. Ukipewa madaraka watendee haki watu wote. Usinyanyase watu kwa sababu una sponsor. Ipo siku sponsor hatakuwepo na utapata tabu sana.
Asante mama kwa kuirudisha nchi kwenye mstari wa haki. Hakika wewe ni zawadi tuliyopewa na Mungu. Tunakuombea ili Mungu mwenyewe awe taa ya njia zako na mwanga wa miguu yako, usiteleze wala kuanguka (Zab 119:105).!

0 Comments