NCHEMBA WATATULIWA MGOGORO WAO
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu, amemaliza mgogoro wa kiutalawa uliodumu kwa muda mrefu na kusababisha kudhorota kwa utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Waziri Ummy amezitaka pande mbili zilizokuwa zinahasimiana, watendaji na madiwani, kuondoa tofauti zao na badala yake kuwa kitu kimoja, kufanya kazi kwa mshikamano, kuheshimiana na kupendana.
Kikao hicho kilichofanyika mapema hii leo chini ya Waziri Ummy, alibaini chanzo cha mgogoro ni mgawanyiko mkubwa kati ya waheshimiwa madiwani, Menejiment ya Halmashauri pamoja na Menejimenti kutokuwa na mshikamano katika utendaji wa kazi.
Sababu nyingine ni ushirikishwaji mdogo wa madiwani kwenye baadhi ya maamuzi ya Halmashauri pamoja na kutokulipwa stahiki zao kwa kipindi kirefu sasa, kitu ambacho kimechochea kuzalisha madeni yanayo athiri Halmashauri kwenye utendajikazi.
Aidha, ukusanyaji mapato usioridhisha wa makusanyo ya ndani na matumizi yasiyo sahihi ya mashine za kukusanyia mapato (POS) pamoja na kuchelewa kupeleka makusanyo Benki na matumizi ya fedha kabla yakufikishwa benki kwanza (Fedha mbichi).
Mhe. Ummy amebaini, upelekaji mdogo wa fedha kwenye miradi ya maendeleo pamoja na kutotumika vema kwa fedha za maendeleo katika shughuli za maendeleo na badala yake fedha zimekuwa zikitumika kwa ajili ya posho za safari, vikao na semina.
Baada ya majadiliano ya muda takribani ni saa mbili, Mhe. Ummy, alitumia fursa hiyo kutoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha, wataalam na madiwani wanafanya kazi kwa ushirikiano bila kuhasimiana miongoni mwao, kwani migogoro haijengi.
Pia amezitaka Halmashauri kuongeza usimamizi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri na kuhakikisha asilimia 40 ya fedha zinazokusanywa zinapelekwa kwenye miradi ya maendeleo ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja kama vile shule, hospitali na masoko.
“Nazikumbushe tena halmashauri zote nchini kuwa, fedha za maendeleo nataka ziende kwenye maendeleo, miradi ile ambayo inatatua changamoto za wananchi moja kwa moja.

Post a Comment