MAHUSIANO YA KUELEKEA NDOA TAKATIFU:
Leo nimepata msukumo kuzungumzia mahusiano kwa kifupi ili tusaidiane hasa wale ambao hatujaingia katika Maisha ya Ndoa.
Nimeona watu wengi sana wakilia juu ya mahusiano baada ya mambo kwenda kombo. Hadi wengine wamemuacha Mungu kwa sababu ya mambo ya mahusiano kwenda ndivyo sivyo.
Ukipata nafasi ya kuzungumza na wanalia juu ya mahusiano utabaini makosa ni yale yale kwa wengi.
Ni muhimu kwako kujiuliza Maswali yafuatayo kabla hujaamua kuingia katika mahusiano na mtu yeyote.
1-Jiulize, Kwa nini uingie katika mahusiano!??
-Mara nyingi watu ukiwauliza sababu za kuingia katika mahusiano huwa hawaelewi sababu za Msingi za kuwa katika mahusiano.
2-Jiulize, Kwa nini uingie katika mahusiano na huyo mtu?
-Lazima ujipe mda wa kutafakari sababu za msingi za kuingia katika mahusiano na mtu fulani.
3-Jiulize, Je malengo yako na huyo mtu unayetaka muwe pamoja mna malengo sawa juu ya mahusiano?
-Ni wazi kuwa kila mtu huwa ana lengo lake ndani yake juu ya kuanzisha mahusiano.
Wapo wanaoamua kuanzisha mahusiano kwa sababu ya kuiburudisha miili na mioyo yao.
Lakini wengine huingia katika mahusiano ili waishi maisha maisha ya ndoa.
Sasa ni muhimu ujue huyo mtu yeye ana mtazamo upi juu ya mahusiano, ikiwa mtakuwa na mtazamo tofauti juu ya mahusiano tarajia kilio katika uhusiano huo.
4-Jiulize, Je ni mda sahihi wa kuwa katika mahusiano?
-Kuna wakati Watu wengi huwa tunaingia katika mahusiano bila kujua ni wakati sahihi au sio.
Unapoingia katika mahusiano kabla ya wakati tegemea matokeo hasi juu ya mahusiano hayo.
Suala la wakati ni muhimu sana kulizingatia sana ili usiende mbele ya wakati.
5-Jiulize, Je Umejiandaa kuishi maisha ya mahusiano?
Maswali hayo yanaweza kukusaidia ili kujenga msingi imara wa kuingia katika mahusiano.
Jifunze kutafakari kabla ya kuchukua hatua ili usijutie maamzi yako.
Asante.
THE LIGHT OF UNIVERSE MINISTRY
Mwl Ejide Andrew Noah
+255743154575.
Muganza, Chato- Geita.
0 Comments