Advertisement

Responsive Advertisement

MAFUNZO YA WATU WAZIMA LEO 24

LESONI, MEI 24

SOMO: NGAO YAKO 



“Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa” (Mwanzo 15:1).



Soma #Mwanzo 15:1—3#. Tafakari muktadha ambapo ahadi hiyo ilitolewa. Kwa nini kauli ya kwanza ya Mungu kwa Abramu ni “Usiogope”? Ni nini ambalo lingalimletea Abramu hofu?



Jambo la kuvutia sana hapa ni kwamba BWANA anamwambia Abramu, “Mimi ni ngao yako.” Matumizi ya kitenzi “mimi” huonesha kuwa BWANA atafanya uhusiano binafsi na Abramu. Mungu atahusiana naye ana kwa ana, uhusiano atakaoufanya nasi pia. 



Utambulisho wa Mungu kama “Ngao” unaonekana hapa kwa mara ya kwanza katika Biblia na ndiyo wakati pekee Mungu alitumia utambulisho huo kujifunua Mwenyewe, japo waandishi wengine wa Biblia wametumia kauli hiyo kumwelezea Mungu (#Kumbukumbu 33:29,# #Zaburi 18:30,# #Zaburi 84:11,# #Zaburi 144:2#). 



Wakati Mungu anapojitaja kuwa ngao ya mtu, je anamaanisha nini? Je kauli hiyo ilikuwa na maana maalumu kwa Abramu ambayo haituhusu sisi leo? Je twaweza kudai ahadi hiyo kwa ajili yetu leo? Je inamaanisha hakuna baya litatupata? Ni kwa jinsi gani Mungu wetu ni ngao? Unaelewaje hali hiyo ya Mungu kuwa ngao yako?



“Kristo hatupendi juu juu bali anatujali na kutupenda kwa upendo imara kuliko ule wa mama kwa mtoto wake. ... BWANA ametununua kwa kuteseka kwake kama mwanadamu, kwa kutukanwa, kunyanyaswa, kudhihakiwa, kukataliwa, na hatimaye kufa. Anakulinda wewe mtoto wa Mungu unayetetemeka. Atahakikisha unakuwa salama chini ya ulinzi wake ..... Udhaifu wetu katika uasili wetu wa ubinadamu hautatukwamisha kumwendea Baba wa mbinguni, kwani Kristo alikufa ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu. " —Ellen G. White, Sons and Daughters of God, uk. 77.



Kwa kila hali, Rolando alikuwa amefahamika kama mfuasi mwaminifu wa BWANA. Ila kwa masikitiko, baada ya muda, kwa ghafla, alifariki dunia. Je waweza kuelezeaje tukio hilo ukizingatia kuwa Mungu ni ngao kwake? Je twapaswa kuelewaje wazo hili la Mungu kama ngao yetu? Elezea. Je, Mungu anaahidi daima kutuepusha dhidi ya kitu gani? (Soma #1 Kor. 10:13.#)

Post a Comment

0 Comments