Advertisement

Responsive Advertisement

MADHARA YA DHAMBI YA UZINZI NA UASHERATI


*MADHARA YA DHAMBI YA UZINZI NA UASHERATI* 😭

Uzinzi utabakia kuitwa uzinzi tu hata kama utafanywa kwa maombi au kwa jina la ucha Mungu, bado utaendelea kuitwa uzinzi.

Uwe wa wazi au wa siri sana, bado unabakia kuwa ni uzinzi tu. Hata ukifanywa na watu wanaotaka kuoana, yaani waliochumbiana, bado haubadiliahwi jina hata kidogo ni UZINZI tu  (uasherati tu).

MATAMKO YA NENO LA MUNGU:

1. Mzinzi, hana akili kabisa, na anaangamiza nafsi yake. (MITH 6:32).

2. Wazinzi na waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu (1KOR 6:9).

3. Kufanya uzinzi ni matumizi mabaya ya viungo vya Kristo, na kujiunganisha na kahaba (1KOR 6:15-16).

4. Watu wa Mungu wasichangamane na wazinzi kabisa (1KOR 5:11).

✍️Uzinzi pia unafukuza roho mpya kanisani, maana wapo wakristo wanatongoza mabinti waumini wapya na wanaliacha kanisa waliloamini ni la Mungu.

✍️ Uzinzi unazuia injili isipokelewe, maana watangaza injili wengi wanazini na watu walio nje ya kanisa kama wanavyozini na walio ndani. Unawezaje kumhubiri mtu unayezini naye? Tuionee huruma injili.

Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Mathayo 5:16

WITO WA MUNGU KWAKO
1KOR 6:18-20;
Ikimbie zinaa, usitende dhambi hiyo kwa mwili wako, kwani mwili wako ni hekalu la Mungu. Wewe ulinunuliwa kwa thamani kubwa, mtukuze Mungu sasa.

 kuna aina nyingi za uzinzi (uasherati) sio mpaka ulale na mwanaume au mwanamke waweza tazama somo hili kwa ufafanuzi zaidi kuhusu aina za uzinzi (uasherati) na namna ya kuziepuka

MUNGU AWE PAMOJA NA KILA MMOJA ANAYEJITIA NIA KUACHANA NA DHAMBI Haraka

Post a Comment

0 Comments