Advertisement

Responsive Advertisement

EPSODE 4 NA KANKWI WA KANKWI

Baada ya kukaa kcmc kama wiki 1 hadi 2 familia yangu iliamua nihamishiwe Dar hospitali ya Muhimbili nakumbuka nilipelekwa na gari ya wagonjwa hadi KIA ndio mara ta kwanza kupanda ndege lkn sasa niliipanda kwa style hio sikuenjoy kiukweli. 

Nikafika Dar nikapokewa na ndugu zangu nikapandishwa kwa gari wa wagonjwa hadi Muhimbili wodi ya sewahaji nafikiri au ile nyingine. 

Sio utani nilikua naogopa sana hofu imenikaa nikatafutiwa kitanda nikalazwa daah nyie hosp sio mahali pa kupazoea wala kukaa yani ww kama ni mzima Mshukuru sana Mungu wako nilikua naona watu wanavyoumwa pale inasikitisha binadam ule uthamani wetu ukifika hosp haupo mimi nawashangaa sana binadam wanaoringa wenye majivuno na kujisikia laiti wangejua ila wacha niwaambie leo kama unaringa acha kama una kiburi acha kama unajisikia acha kwasababu iko siku..

Basi nikakaa pale wodini sasa kwa sababu ya ile hofu wagonjwa ni wengi sielewi ilibidi niwe namuomba nurse awe anakaa jirani na mimi usiku kama mlinzi na yule nurse alinielewa sana Mungu ambariki huko aliko. 

Baada ya kukaa kama wiki hivi nikahamishiwa wodi ya Moi.

Unajua unapopata hii tatizo la Uti wa mgongo kuna changamoto kama tatu hivi zinatokea tu automaticaly( 1)kiafya kuna mambo yanatokea(2)changamoto ya kimahusiano(3) familia wanawaza nini kifanyike hapo swala hasa la uchumi ili kumtibu mtu.

Tuanze na changamoto ta kiafya inayotokea ni hivi ukiumia uti wa mgongo kwa kesi kama yangu ( C6,C7)kwanza unapooza ukishapooza inamaana mikono miguu haifanyi kazi,pia kupata haja ndogo na kubwa kwa kawaida ni tatizo haviwezekani kinachofanyika wanakuwekea mpira wa mkojo lakini pia unavalishwa pampers kwa ajili ya haja kubwa na ikitokea hata hujui wala kuhisi yani hiki kipindi kiliniharibu akili nilikuwa sijiamini kanisa ( self esteem yangu ilikua chini ) sikuwa na ujanja nilikua mtu wa hasira sanaa kila kitu nahisi kama naonewa. Basi ikaenda hivo nikakaa Moi mpaka niliitwa Balozi kwasababu nilikaa mda mrefu nakumbuka hata kuona nje sikuwahi mimi ni ndani tu akija mgonjwa atatibiwa ataondoka mimi nipo ilinivuruga sana ( pychologically was not ok kabisa. 

Kuna siku walikuja darasa langu la Mweka walitokea Hunting Selous game reserve ndio

Post a Comment

0 Comments