Advertisement

Responsive Advertisement

EPSODE 4 NA KANKWI WA KANKWI

Walivyokuja Moi kunitembelea ndio nikaomba wanitoe nje kwenye korido ili niweze kuwasalimu nilifurahi sana hio siku na nilibahatika hata kuona jua nje na kupata fresh air. 

Kuna wakati mwili ulikuwa unawaka motooo sana nikaomba niwe nawashiwa AC mpaka mwisho yani ukija chumba nilichokuwepo unaweza kuhisi ni chumba cha maiti kwasababu ya baridi niliambia huo moto ni ganzi inaachia taratibu. 

Nakumbuka daktari alisema kwa injury yangu kulikuwa hakuna ulazima sana wa kwenda Nje kutibiwa bali mazoezi na kujipa mda itapona basi nikaliamini hilo.

Tukapata ruhusa tukarudi nyumbani ndipo dada angu kipenzi anaitwa Idda na familia yake wakachukua jukumu la kunilea na kunitunza nyumbani kwake. 

Kumbuka natoka moi bado hali yangu ni mbaya yani kukaa bado mimi ni kulala tu 24/7 natumia hio mipira ya mkojo natumia pampers na bahati mbaya nilipata vidonda ( bed sore) hivi vidonda ni vibaya vinatisha vilinichimba sehem za makalio na kwenye mapaja kwahio tukawa tunatibu vidonda na hio hali ya kupoza mwili.. 

Tumehangaika sio siri kutafuta tiba zote dunia hii naambiwa dave huwezi jua uponyaji wako upo wapi basi kila ukiambiwa sehem flani ipo dawa basi dada angu na mume wake wanaitafuta napewa.. kiukweli ilifika kipindi nilikata tamaaa kabisa na hii ni baada ya mwaka unaofuata kumpoteza dada angu kwa ajali ya gari huko uganda na mwaka huo huo kumpoteza baba angu niliumia sana na kupoteza matumaini ya kuishi. 

Hamu ya kula haikuwepo yani nakumbuka nilikuwa nakula ugali maziwa mgando na soda basiii vingine havipandi jitahidi lkn wapi.
Kwenye msiba wa baba sikuruhusiwa kusafiri umbali mrefu ila nililazimisha kwenda kumzika baba kijijini nikasema potelea mbali lkn nilifika salama nikamzika baba nikarudi Dar kuendelea na mapambano....itaendelea

Post a Comment

0 Comments