Advertisement

Responsive Advertisement

BAJETI YA UTAFITI NCHINI KUONGEZWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuongeza Bajeti ya Utafiti kuanzia mwaka wa Fedha 2021/22.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyofanyika Chuoni hapo, ambapo amesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha utafiti na kuendeleza ubunifu Nchini ili uweze kubiasharishwa, kutumika katika Viwanda na hatimae kuchangia Uchumi wa Nchi.

"Nimeona ubunifu na tafiti zinazofanywa na vijana wetu kuanzia wiki mbili zilizopita pale Dodoma MAKISATU, Serikali inaahidi kuwekeza zaidi katika kuwaendeleza, hivyo naagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na kuwa Bajeti yenu imepita mfanye mapitio na kuongeza Bajeti katika eneo hilo ili tafiti hizi na ubunifu uwe na tija kwa Taifa letu," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Post a Comment

0 Comments