Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 22

KESHA LA ASUBUHI

Jumamosi 22/05/2021

*MCHAKATO WA UTAKASO*

*Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.* Waebrania 2:18 

💎 Nimeamshwa saa sita kamili ili niandike maelekezo ambayo nimepewa... Maneno yaliyozungumzwa, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Ukiwasha nuru ya moyo wako kutoka katika hekima za wanadamu, itazimika gizani. Tafuta hekima yangu, nawe utaongozwa na mshauri asiyekosea. Mwongozo huu ni upendeleo kwa kila mtoto wa Mungu kuwa nao. Omba nawe utapokea; bali omba ukiamini kwa imani. Ombea kile ambacho ni sawa sawa na Neno la Mungu. Amini, nawe utapokea. 

💎 Kristo ni chanzo cha nguvu zetu. Hebu tujifunze mafundisho yake. Kwa kumtoa Mwana wake wa pekee ili aishi katika ulimwengu wetu na kuwekwa katika majaribu ili aweze kutufundisha jinsi ya kushinda, Baba ametupatia msaada ili tusiweze kuchukuliwa mateka na yule mwovu. Kukutana na adui aliyeanguka, Kristo alimshinda kwa niaba ya wanadamu. Alijaribiwa kwa kila namna kama sisi tunavyojaribiwa, lakini aliyapinga majaribu kwa uwezo wa kiungu, ili aweze kutusaidia wakati tunapokuwa tumejaribiwa.

💎 Kuwa washirika wa asili yake ya uungu, tunapaswa tujifunze kuyatambua majaribu ya Shetani, na katika nguvu ya neema Yake, tuushinde uharibifu uliopo ulimwenguni kupitia tamaa. Yule ambaye wakati fulani alikuwa mwanadamu mwenye dhambi anaweza kusafishwa na kutakaswa kupitia haki ya Kristo, na kusimama mbele ya wanadamu wenzake kama mtendakazi pamoja na Mungu. Kwa mtu anayemtafuta Mungu kwa bidii, hakika atapewa asili ya kiungu, upendo wa Kristo hakika utatolewa kutoka moyoni.... 

💎 Shetani anafanya kazi kwa werevu wote ili kuzishambulia roho. Je, tunapaswa kufanya nini? Hebu tuamini kwamba Bwana yupo radhi kusimama na kuwatia moyo walio dhaifu. 

🔘 *Utapata nguvu yako kubwa zaidi katika kukaa katika kila ambacho ni cha kiroho. Hebu utakaso wa ukweli wa Neno la Mungu ufunuliwe katika maisha yako. Hebu acha wakala huyu aisafishe na kuiinua roho. Bwana angependa kuwa na watumishi wake wanaomtumikia watembee kwa unyenyekevu mbele Yake. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.” (Mathayo 11:29, 30).*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

Post a Comment

0 Comments