*KESHA LA ASUBUHI*
*Jumatatu 17/05/2021*
*UTAKATIFU WA MOYO*
“ _Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA, Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu._ "
Yeremia 31:33
▶️ Sheria ya Mungu inapoandikwa moyoni itaonekana katika maisha safi na matakatifu. Amri za Mungu sio maneno yaliyokufa. Ni roho na uzima, yanayafanya mawazo na fikra kufuata mapenzi ya Kristo. Katika moyo ambamo yameandikwa yatatunzwa kwa jitihada zote; maana kutokana na hayo kuna mambo ya uzima.
▶️ Wote ambao wanampenda Yesu na kutunza amri zake wataepuka mwonekano wa uovu; si kwa sababu wamelazimishwa kufanya hivyo, bali kwa sababu wana kila mfano safi, na kujihisi kuepuka wakikutana na kitu chochote kinachopingana na sheria iliyoandikwa mioyoni mwao. Hawatahisi kujitosheleza, bali tumaini lao litakuwa kwa Mungu, yeye pekee ambaye anaweza kuwaepusha na dhambi na uchafu. Angahewa linalowazunguka ni safi; hawataharibu nafsi zao au nafsi za wengine. Ni furaha yao kufanya mambo kwa haki, kupenda rehema, na kuenenda kwa unyenyekevu mbele za Mungu.
▶️ Hatari iliyopo mbele ya wale wanaoishi katika siku hizi za mwisho ni kutokuwepo dini halisi, kutokuwepo utakatifu wa moyo. Uwezo wa Mungu uongoao haujatumika katika kubadilisha tabia zao. Wanadai kuuamini ukweli mtakatifu kama taifa la Wayahudi lilivyofanya; lakini katika kushindwa kwao kuutekeleza ukweli, wanakuwa wajinga wa Maandiko na uwezo wa Mungu. Uwezo na ushawishi wa sheria ya Mungu unawazunguka, lakini si ndani ya roho kuihuisha katika utakatifu wa kweli...
▶️ Mungu amekusudia kwamba mwalimu wa Biblia katika tabia na maisha ya nyumbani awe mfano wa kanuni za ukweli ambao anaufundisha kwa wanadamu wenzake.
▶️ *Vile mtu alivyo hutoa ushawishi mkubwa kuliko kile anachosema. Maisha ya utauwa, matulivu, yasiyobadilika ni barua iliyo hai, inayojulikana na kusomwa na watu wote. Mwanadamu anaweza kuzungumza na kuandika kama malaika, lakini matendo yake yanaweza kufanana kama malaika walioanguka... tabia ya kweli si kitu ambacho kinajengwa kutokea nje, au kuvikwa, bali ni kitu ambacho kinatokea ndani. Ikiwa wema wa kweli, usafi, upole, unyenyekevu, na usawa, haya yote yakikaa ndani ya moyo yataakisiwa katika tabia; na tabia hiyo itakuwa na nguvu kamili.*
0 Comments