AKIDAOG1 AMZAWADIA MKE WAKE GARI MWIJAKU AELEZEA

JIFUNZENI-Leo naomba niongee kama DC ni haki yangu kukosoa na kusifia . Huyu bwana anaitwa @akidaog1 .

Mtanzania mnyenyekevu mfanya biasharaa . Ndie mwanaume wa kwanza Tanzania kumzawadia mwanamke wake gari ambalo limesajiliwa kwa jina la mwanamke wake .

Tumezoea kuona vijana wanakopa magari kisha wanapiga na kelele nyingiii mnoo . Ili waonekane ..! Tazama mwanaume huyu @akidaog1 kimya kimya kama JMOO

S/O kwa @akidaog1 Mtanashati mwenye kuthamini wake zakeeee..!

Kupitia ndoa za @akidaog1-Linapokuja suala la kuwa na life partner Oa/olewa na mtu ambae unampenda kwa moyo wote. Kamwe usijidanganye kufunga ndoa na mtu ambae haumpendi kwa kisingizio kuwa utajifunza kumpenda.

Love is all about Feelings. Mapenzi sio LEARNING INSTITUTION, ukiyageuza kuwa Mtaala huwezi ku-graduate hata Certificate Course!

Pata mtu ambae atakuchangamsha kihisia na kiakili. Mtu ambae hataubadilisha ule ubora ulionao, bali atakuongezea thamani na kuwa bora zaidi...

Hakuna kitu kizuri kama kuwa mkweli wa nafsi yako. Funga ndoa na mtu aliye kama rafiki kwako. Mtu ambae utaweza ku-share nae vitu vyako vidogo vidogo vya kila siku mpaka mipango mikubwa ya maisha yako.

Mtu ambae utatamani uwe nae kila mwisho wa siku na mwanzo wa siku. Usioe/kuolewa kwa sababu unafikiri tu muda wako umefika, bali fanya hivyo kwa sababu umepata mtu sahihi bila kujalisha kiasi gani muda umeenda.

Mtu ambae ana roho nzuri, mtu ambae haogopi kukuonesha wazi ni namna gani anakupenda. Mtu ambae anakutia moyo. Umpatapo mtu wa aina hii, kuwa mkweli kwake. Onesha shukrani kwa Mungu na mpende siku zote za uhai wako mtu huyu ambae amekupa zawadi ya ku-share maisha yake na wewe!

No comments