WINO WA JACKSON SILLO
Historia yake katika soka la Afrika ni ya kuvutia na yenye harufu ya NUNI lakini si iliyo na mafanikio makubwa sana
1. Libya aliinoa klabu ya Al-Ahli Benghazi akiwa kama Kocha mkuu.
Alidumu kwa miezi 8 tu, kutoka Aprili hadi Disemba 2013
2. Sudan alizinoa klabu mbili kwa nyakati tofauti tofauti.
Alianza na Al-Hilal ambapo alidumu kwa miezi 4 tu akiwa kama Kocha mkuu, kutoka Disemba 27, 2013 hadi Aprili 30, 2014
Mapema mwaka huu aliiongoza Al -Merrikh katika hatua ya makundi alipochukua nafasi ya Didier Gomes da rosa ambaye kwa sasa yupo Simba SC
Klabuni hapo amedumu kwa mwezi 1 na wiki 3 tu, kutoka Januari 28 hadi Machi 7, 2021
3. Misri aliinoa klabu ya Ismaily akiwa kama Kocha mkuu.
Alidumu kwa siku 22 tu, kutoka Januari (4-26) 2016
4. Italy aliinoa klabu ya daraja la tatu Serie D, Pont Donnaz Hone Arnad akiwa kama Kocha mkuu
Alidumu kwa miezi 4 na siku 20, kutoka Julai 1 hadi Novemba 22, 2019
NOTE YAFUATAYO
1. Kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya, si Kocha mwenye historia wala mafanikio kabisa
2. Ninachoamini kinaweza kuwa msaada kwa Yanga ni kupitia uzoefu alionao na soka la Afrika plus UGHAIBUNI
3. Ukitoa ubora wa Kocha lakini matokeo mazuri ya timu huchagizwa pia na viwango bora vya wachezaji
-Sio kila matukio uwanjani yataamuliwa na mbinu za Mwalimu, mengine ni uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja
-Kwa Yanga wasitegemee sana mabadiliko ya haraka, bado Uongozi unapaswa kusajili wachezaji bora zaidi
Huu Wino acha uishie hapa, nisichafue karatasi hii moja niliyopewa kukuwasilishia haya
AHSANTENI ."
0 Comments