Advertisement

Responsive Advertisement

VUNJABEI ASHINDA TENDA, KUTENGENEZA JEZI ZA SIMBA SC

MKATABA WA MIAKA MIWILI YENYW THAMANI YA TSH. BILIONI 2 IMETOSHA KWA FRED VUNJABEI KUTENGENRZS JEZI MSIMBAZI

Mfanyabiashara maarufu wa mavazi nchini @fred_vunjabei ameshinda tenda ya kutengeneza jezi na vifaa vya michezo vya Simba kwa mkataba wa miaka miwili yenye thamani ya Sh 2 bilioni.

Akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari, Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema #Fred ameshinda tenda hiyo baada ya kushindanishwa na makampuni 11 kutoka nchi mbalimbali.

#Barbara amesema mchakato wa kupata kampuni itakayo tengeneza jezi pamoja na vifaa mbalimbali  vya michezo vya Simba ulianza Desemba mwaka jana ukihusisha makampuni makubwa Duniani.

Naye @fred_vunjabei ameishukuru Simba kwa kumwamini na kumpa tenda hiyo huku akiahidi kutoa vifaa vyenye ubora mkubwa.

"Nashukuru Simba kuwa kuniamini kama kijana na mtanzania ambaye nilikuwa nashindana na makampuni makubwa kutoka nje, ikiwemo Afrika Kusini.

"Licha ya kushinda kutengeneza jezi na vifaa vya michezo pia Simba wametupa mamlaka ya kusimamia matukio yote ya klabu hiyo," amesema Vunjabei.

Post a Comment

0 Comments