Advertisement

Responsive Advertisement

TUISILA KISINDA NA DICKSON JOB WALIOPATA MAJERUHI DHIDI YA MECHI YA GWAMBINA, WANAENDELEA VIZURI

Daktari wa klabu ya Yanga Dkt. Mngazija amethibitisha kuwa wachezaji wawili (Kisinda & Dickson Job) ambao walishindwa kuendelea na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Gwambina Fc wanaendelea vizuri.

Mngazija amesema Kisinda aliangukia bega lililomfanya apate maumivu makali lakini hakuna madhara makubwa hivyo anaendelea na matibabu.

Kuhusu Dickson Job Mngazija amesema waliamua kumtoa ili asipate majeraha makubwa ambayo yangeweza kusababisha madhara makubwa, hivyo nae anaendelea vizuri na leo jioni watawafanyia vipimo vya mwisho watakaporejea kambini.

Post a Comment

0 Comments