Advertisement

Responsive Advertisement

TMA: KIMBUGA JOBO KIMEPUNGUA NGUVU

Weather Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) @tanzaniameteorological imetoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga 'JOBO" kilichopo bahari ya Hindi umbali wa kilomita 200 mashariki mwa kisiwa cha Mafia.

TMA imesema kimbunga Jobo kimepungua nguvu kwa haraka baada ya kuingia katika mazingira yenye mzunguko wa upepo kinzani.

Taarifa ya TMA @tanzaniameteorological imesema kuwa kwa sasa kimbunga hicho ni hafifu.

Kimbunga hafifu 'JOBO' kinatarajiwa kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo machache hususani ya ukanda wa Pwani kadri kinavyosogea nchi kavu kwa siku ya leo Tarehe 24 na kesho Aprili 25, 2021. Pia mamlaka hiyo imetoa tahadhari kuwa uwepo wa kimbunga hicho hafifu utasababisha mawimbi makubwa baharini.

Maeneo yanayotarajiwa kupata athari ya moja kwa moja ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Kisiwa cha Unguja.

Wananchi wanashauriwa kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments